#Football #Sports

LEOPARDS WAREJEA UONGOZINI KPL

Miamba wa soka nchini AFC Leopards wamerejea uongozini mwa ligi kuu ya soka KPL kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nairobi United ugani Nyayo, na kupanda juu ya washikilizi wa rekodi ya ubingwa Gor Mahia kwa pointi 1.

Naibois walijifunga bao kunako dakika ya 20 kabla ya Ingwe kufunga bao la pili kunako dakika ya 70 kupitia kwa Kelly Madada.

Ingwe sasa wana pointi 27, 1 mbele ya Gor Mahia ambao wamecheza mechi 2 chache ikilinganishwa na Ingwe.

Hata hivyo, Leopards watapata fursa ya kupanua mwanya wa pointi watakapochuana na Tusker FC Jumamosi kabla ya Gor kucheza mechi yao dhidi ya Shabana Jumapili.

Naibois ambao wanajiandaa kuendelea na mechi za CAF Confederations Cup, wanasalia katika nafasi ya 9 wakiwa na pointi 19, huku wakijivunia mechi 3 mkononi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

LEOPARDS WAREJEA UONGOZINI KPL

TRUMP: NITAIENDESHA VENEZUELA

LEOPARDS WAREJEA UONGOZINI KPL

GUARDIOLA APOTEZA TUMAINI EPL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *