PROF. OKOWA ACHAGULIWA JAJI ICJ
Kenya imepiga hatua kubwa kwenye ngazi ya haki ya kimataifa baada ya Profesa Phoebe Okowa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa kuwa jaji katika mahakama ya kimataifa kuhusu haki ICJ.
Profesa Okowa ambaye tayari ni mwanachama wa tume ya sheria ya kimataifa, amechaguliwa katika kura za baraza kuu la umoja wa mataifa UN na baraza la usalama, na sasa atachukua wadhifa ulioachwa na hakimu Abdulqawi Yusuf wa Somalia.
Okowa atakuwa mwanamke wa kwanza mkenya kuhudumu kwenye mahakama hiyo ya ICJ.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































