SIFUNA APINGA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA AJENDA 10
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amepuuza madai kwamba ajenda ya vipengele kumi kati ya chama cha ODM na serikali ya Kenya Kwanza imetekelezwa.
Sifuna amesema kamati iliyokuwa ikisimamia utekelezaji wa ajenda hiyo ilishindwa kuwasilisha ripoti yake ya mwisho kufikia tarehe ya mwisho ya Machi 7, na badala yake ikatoa maelezo kwa kundi dogo katika kile alichokiita maigizo.
Sifuna amesema kamati hiyo ilipaswa kutoa ripoti za maendeleo kila baada ya miezi miwili na kuwasilisha ripoti kamili kwa umma kufikia Machi 7, tarehe ambayo pia amedai ndiyo iliyokuwa mwisho wa makubaliano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































