UCHUNGUZI: KWS NDIO WALIKUWA WA MWISHO NA ODHIAMBO
Mchakato wa kupata haki kwa familia ya mvuvi aliyetoweka katika mbuga ya wanyamapori ya Lake Nakuru Brian Odhiambo umeanza kupata mwelekeo, afisa wa polisi anayechunguza tukio hilo Julius Muhuri akiwatambua maafisa 6 wa KWS kama watu wa mwisho walioonekana na Odhiambo kabla ya kutoweka kwake.
Afisa huyo ameiambia mahakama kwamba kulingana na uchunguzi, signal ya simu ya Odhiambo ilikuwa karibu na washukiwa wakati wa kukamatwa kwake kwa tuhuma za kuingia katika mbuga hiyo kinyume na sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































