WAKENYA WALIOKWAMA MYANMAR WAREJESHWA
Hatimaye wakenya 119 waliookolewa nchini Myanmar baada ya kulaghaiwa mtandaoni kupewa ajira wamerejeshwa humu nchini, serikali ikisema juhudi za kuwarejesha wakenya wengine 200 ambao wamekwama nchini humu zinaendelea.
Kupitia taarifa, wizara ya masuala ya kigeni imesema 119 hao waliachiwa huru kutokana na operesheni ya vikosi vya usalama vya Myanmar dhidi ya makundi yanayoendeleza uhalifu karibu na mpaka huo na Thailand.
Serikali imewatahadharisha wakenya dhidi ya ahadi za ajira ghushi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































