#Football #Sports

MATANO AKOSOA USIMAMIZI, WACHEZAJI WAKE

Kocha mkuu wa klabu ya KCB Robert Matano, amewalaumu wasimamizi wa mechi ya jana kati ya timu hiyo na Nairobi United ambako timu yake ilishindwa kupata pointi 3 muhimu, akisema mwamuzi aliwapa Naibois penalti isiyofaa.

Kwenye kikao na wanahabari baada ya mechi hiyo iliyoishia sare ya bao 1-1, amesema hali hiyo iliwanyima vijana wake ushindi muhimu.

Aidha, mkufunzi huyo amewalaumu wachezaji wake hasa washambulizi, kwa kukosa kumalizia nafasi za wazi mbele ya lango.

Matano ameeleza kushindwa kuelewa ni vipi washambulizi walipoteza nafasi hizo, anazosema zilikuwa rahisi kufungwa.

Kulingana na Matano, wachezaji wake walikosa hamu ya kufunga mabao mbali na kukosa kuelewa walichokuwa wakifanya uwanjani.

Kutokana na sare hiyo, KCB walipanda nafasi moja hadi nafasi ya 8 juu ya Bandari FC, huku Naibois wakisalia katika nafasi ya 10.

Katika mechi ya pekee hii leo, viongozi Gor Mahia wana fursa ya kurejesha mwanya wa pointi 9 iwapo wataandikisha ushindi dhidi ya Posta Rangers.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MATANO AKOSOA USIMAMIZI, WACHEZAJI WAKE

NG’ENO, WENGINE 5 KUPEWA BURIANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *