WAZIRI RUKU AKASHIFU MADAI YA ALIYEKUWA NAIBU RAIS YA KUWAHUSISHA WASHIRIKA WAKE NA GHASIA ZA UCHAGUZI
Waziri wa utumishi wa umma,Geoffrey Ruku, amepuuza madai ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kuhusisha washirika wake na vitisho vya ghasia za uchaguzi.
Ruku amekashifu madai hayo kuwa matamshi ya chuki yanayochochewa kisiasa na yanayolenga kumharibia sifa zake.
Hayo yanajiri baada ya Gachagua kuandika barua akitaja kanda ya video ambapo watu watatu – Simon Njagi Njiru, Josiah Kariuki Ngari, na Susan Nyaga – walidaiwa kumtishia yeye na wakaazi wa eneo bunge la mbeere kaskazini.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































