FKF YAZINDUA ZOEZI LA KUTAFUTA VIPAJI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA LA U17 2027
Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limezindua zoezi lake la kutafuta vipaji kwa ajili ya kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka 2027 huku zoezi la kwanza la uchunguzi likipangwa kufanyika siku ya Jumapili katika eneo la Ndhiwa, Kaunti ya Homa Bay.
Lengo kuu la zoezi hilo ni kuwatafuta wavulana waliozaliwa mwaka 2011, katika juhudi za FKF kote nchini za kubaini na kulea kizazi kijacho cha wachezaji wa soka wa Kenya.
Wachezaji watakaochaguliwa wataingia katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo, unaojumuisha elimu rasmi pamoja na mafunzo ya kiwango cha juu katika chuo cha kwanza cha soka cha makazi nchini Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































