WANAFUNZI WARUSHIWA KIBARUA KUREJEA VYUONI
Kibarua sasa ni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma kurejea vyuoni baada ya wahadhiri wao kusitisha mgomo wa siku 49 uliokuwa umelemaza masomo na kusababisha maelfu ya wanafunzi kurejea makwao.
Mgomo huo umesitishwa baada ya wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu kukubali kulipwa deni lao la shilingi bilioni 7.9 kwa awamu mbili jinsi serikali ilivyopendekeza.
Aidha, serikali imeahidi kuanza mazungumzo mara moja kuhusu mishahara yao kwenye mktaba wa maelewano wa mwaka 2025-29.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































