POLISI WALIOREJEA WATAJA UFANISI
Maafisa wa polisi waliorejea nchini kutoka Haiti wametaja kufanikiwa kwa misheni yao ya kurejesha utulivu katika taifa hilo la Karibia, mojawapo ikiwemo kufungua upya barabara kuu zilizokuwa zimetekwa na magenge ya wahalifu.
Wakizungumza siku moja baada ya kurejea, maafisa hao wameelezea kupitia changamoto mbali mbali katika muda wa miezi 18 waliyohudumu nchini humo.
Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, amewataka kutumia ujuzi waliopata katika operesheni zijazo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































