DE BRYUNE AFANYIWA UPASUAJI
Kiungo wa kati wa klabu ya Napoli Kevin de Bryune amefanyiwa upasuaji wa msuli katika eneo la Antwerp nchini Ubelgiji baada ya kupata jeraha la msuli yaani hamstring alipocheza mkwaju wa penalti katika ushindi wao dhidi ya Inter Milan mwishoni mwa wiki.
Katika taarifa, Napoli imetangaza kwamba upasuaji huo wa hapo jana ulikamilika salama, na kwamba huenda raia huyo wa Ubelgiji akawa nje kwa kati ya miezi 3-4 kutokana na upasuaji huo.
De Bryune mwenye umri wa miaka 34, amewafungia mabingwa hao wa Serie A mabao 4 tangu kuwasili kutoka Manchester City mapema msimu huu, akifunga mara 3 kupitia mikwaju ya penalti na mara moja kupitia ikabu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































