KPA YAFUZU LIGI YA AFRIKA LICHA YA KUPIGWA NA MAPUTO
Timu ya mpira wa kikapu ya Kenya Ports Authority (KPA) imejihakikishia kufuzu katika mashindano ya Basketball League Africa yanayoendelea Misri, licha ya kupoteza 91–76 dhidi ya mabingwa watetezi Ferroviario de Maputo kwenye mechi ya mwisho ya Kundi B.
KPA ilikabiliana vikali na wenyeji waliokuwa na wachezaji sita wenye uzoefu mkubwa ikicheza kwa ujasiri na kasi sawa katika hatua zote za mchezo.
Hata hivyo, Maputo walivunja upinzani wa KPA katika robo ya mwisho, lakini matokeo ya awali yakawawezesha wawakilishi hao wa Kenya kufuzu kwa hatua inayofuata ya mashindano.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































