GACHAGUA ASEMA RUTO LAZIMA AONDOKE 2027
Aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, amepuuzilia mbali mjadala unaoendelea kuhusu nani atakayekuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027, akisema mjadala huo hauna maana.
Gachagua amesema mjadala huo unalenga kupotosha Wakenya, hasa kutoka eneo la Mlima Kenya, na kuondoa umakini wao katika masuala muhimu yanayowahusu.
Aidha, ameongeza kuwa iwapo Ruto atamchagua Gladys Wanga au Oburu Oginga kuwa mgombea mwenza wake, Wakenya hawana nia na hilo, akisisitiza kuwa lengo lao kuu ni kumng’oa madarakani mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































