#Football #Sports

KANYI AIAMINI HARAMBEE STARLETS WAFCON

Aliyekuwa kocha wa Harambee Starlets, Richard Kanyi, ameonyesha imani kubwa katika nafasi ya Kenya kung’ara kwenye Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wanawake ya mwaka 2026.

Kanyi, aliyeinoa timu hiyo kati ya Agosti 2017 na Machi 2018 na pia kuiongoza Thika Queens kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2016/2017, amepongeza Shirikisho la Soka nchini pamoja na serikali kwa kuwekeza katika maandalizi ya kimataifa kuelekea mashindano hayo.

Starlets wanatarajiwa kusafiri kuelekea Abidjan Februari 28 kwa mechi mbili za kirafiki za kimataifa. Watacheza dhidi ya Benin Machi 2 na wenyeji Ivory Coast Machi 4, mechi zitakazochezwa katika Uwanja wa Olimpiki wa Alassane Ouattara.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *