#Business

USHURU WA KAUNTI, SHERIA ZA SEHEMU MBALI MBALI ZALEMAZA SEKTA YA USAFIRI

Wito umetolewa kwa serikali kuweka mikakati ya kuoanisha  kwa haraka ushuru wa lori za kaunti na kukagua sheria zinazozuia uchukuzi ili kuongeza ufanisi na ushindani katika sekta ya usafiri wa barabarani kufuatia ripoti mpya ya Mamlaka ya Ushindani ya Kenya (CAK) na Benki ya Dunia.

Tathmini hiyo aidha inaonyesha kuwa serikali ya kenya inafanya vyema ikilinganishwa na mataifa mengine ya  kipato cha kati, sekta yake ya usafiri wa barabarani bado inazuiliwa na gharama iliyogawanyika katika ngazi ya kaunti na vizuizi vikali kwa wasafirishaji kutoka nje.

Wasafirishaji wanakabiliwa na mahitaji ya leseni, maegesho, mizani na utekelezaji ambao unatozwa kwa kujitegemea na kaunti, na hivyo kusababisha gharama zisizotabirika za kufuata. Ada za ushuru na vibali maalum huathiri vibaya waendeshaji wanaosafirisha bidhaa kama vile bidhaa za kilimo na nyinginezo.

Hata hivyo imebainika kuwa malalamishi yalioibuliwa mwaka wa 2019 na Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini (KNCCI) bado hayajatatuliwa, huku kusimamishwa kwa hivi majuzi kukifanya Chama cha Wasafirishaji wa Kenya (KTA) kuwasilisha ombi kwa Rais huku kukiwa na ongezeko la gharama na kutotekelezwa kwa sheria.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

USHURU WA KAUNTI, SHERIA ZA SEHEMU MBALI MBALI ZALEMAZA SEKTA YA USAFIRI

TAHARUKI NAROK TOWNSHIP

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *