#Football #Sports

BAYERN WATAISHINDA PSG ASEMA NEUER

Kipa mkongwe wa Bayern Munich, Manuel Neuer, amesema
kwamba timu yake inajua jinsi ya kuumiza mabingwa watetezi
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris Saint-Germain (PSG),
watakapokutana hii leo katika michuano hiyo
PSG walitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka jana katika
uwanja wa Allianz Arena wa Bayern, baada ya kuichapa Inter
Milan mabao 5–0.
Hata hivyo, Bayern wanashuka Parc des Princes wakiwa katika
hali nzuri, baada ya kushinda mechi zote 15 walizocheza msimu
huu katika michuano yote — rekodi ya mwanzo bora zaidi katika
ligi kuu tano za Ulaya.
Katika Michuano Mingine ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya
Liverpool watachuana na Real Madrid katika Uwanja wa Anfield

huku Arsenal wakiwa ugenini kuchuana na Slavia Praha,
Tottenham watakua nyumbani kuwakaribisha Copenhagen,
Napoli wakipige dhidi ya Frankfurt, Juventus wavaane koo na
Sporting, Atletico Madrid dhidi ya Union St. Gilloise, Olympiacos
dhidi ya PSV huku Bodo Glimt wakiwaalika Monaco, Villareal
nao watakua Ugenini Kuvaana na Pafos.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

BAYERN WATAISHINDA PSG ASEMA NEUER

WAVUNJAJI WA SHERIA ZA MITIHANI WANASWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *