WANAFUNZI TRANS MARA SOUTH SHULENI
Hatimaye wanafunzi katika shule ya Sitet Comprehensive eneo la Trans Mara South wamepata fursa ya kurejea shuleni kwa muhula wa kwanza baada ya maafisa wa usalama kuwaondoa watu waliokuwa wakiishi kwenye shule hiyo.
Operesheni hiyo iliongozwa na chifu wa Olodonyo-Orok Paul Rutto, mkurugenzi wa elimu eneo hilo George Muchina akiripoti kuwa wanafunzi wapatao 250 waliripoti katika shule hiyo hapo jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































