TAREHE YA KESI YA OJWANG YAPANGWA
Kesi ya mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang aliyeuawa katika kituo cha Central Police jijini Nairobi itaanza kusikilizwa tarehe 12 Januari mwaka ujao, upande wa mashtaka ukitegemea ushahidi kutoka kwenye kanda ya CCTV kuthibitisha kesi dhidi ya washukiwa.
Miongoni mwa washtakiwa kwenye kesi hiyo ni aliyekuwa OCS wa kituo hicho Samson Taalam na maafisa wengine, huku mashahidi 6 dhidi yao wakiwa tayai chini ya ulinzi wa serikali.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 15 mwezi ujao ambapo ushahidi zaidi utawekwa wazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































