IEBC YAMTEUA SUNKULI KUWA KAIMU CEO
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imemteua Moses Ledama Sunkuli kuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Katibu wa Tume.
IEBC imesema kuwa Sunkuli, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Operesheni za Uchaguzi, atahudumu kwa nafasi ya kaimu kwa kipindi cha miezi sita au hadi mchakato wa kuajiri afisa mkuu mtendaji wa kudumu utakapokamilika.
Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Marjan Hussein Marjan kujiuzulu kufuatia makubaliano ya pande zote ya kusitisha huduma zake katika tume hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































