MILIMU ASEMA LEOPARDS WANA UWEZO WA KUBEBA TAJI
Aliyekuwa Meneja wa AFC Leopards, Joseph Milimu, ameitaka klabu hiyo yenye mataji 12 ya ligi
kuanza kujiamini kuwa ina uwezo wa kutwaa ubingwa wa KPL msimu huu.
Milimu amesema ushindi wa 1-0 wa Ingwe dhidi ya Gor Mahia katika Mashemeji Derby ulikuwa
tamko la nia, akisisitiza kuwa kikosi cha kocha Fred Ambani kina msingi madhubuti wa kuanza kupata
matumaini ya ubingwa.
Aidha, Milimu ameongeza kuwa hakuna timu iliyoonyesha ubabe wa moja kwa moja msimu huu,
jambo ambalo linawapa mabingwa watetezi, Police FC, nafasi nzuri ya kutetea taji lao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































