#Football #Sports

AKONNOR AKUBALI KUWAJIBIKIA MATOKEO DUNI

Kocha mkuu wa Gor Mahia Charles Akonnor amesema yuko tayari kuwajibikia matokeo duni yaliyoandikishwa na kalbu hiyo hapo jana, baada ya kupokezwa kibano cha magoli 4-1 na APS Bomet kwenye mechi ya ligi kuu KPL.

Kutokana na maandalizi ya Mashemeji Derby wikendi hii, Mghana huyo alifanya mageuzi 9 kwenye kikosi kilichoizamisha Tusker FC 1-0 bila Jumamosi iliyopita, na licha kuwaleta wachezaji wake tegemezi katika kipindi cha pili, uharibifu ulikuwa tayari umetekelezwa na hawakuweza kuokoa hali.

Licha ya George Amonoo kuwaweka Gor kifua mbele dakika ya 5, mabingwa hao mara 21 walitolewa rangi na maafande, Hansel Ochieng akifuta uongozi dakika ya 40 kupitia mkwaju wa penalti na kuwakabidhi APS Bomet utawala kwenye mechi katika dakika ya 43.

Philip Wasai alijifunga bao dakika ya 76 na kufanya mambo kuwa 3-1, kabla ya Rodgers Kipkemoi kuwahakikisha APS ushindi kunako dakika ya 87, baada ya kumegewa pasi na Ochieng.

Akizungumzia matokeo hayo ambayo ambayo ni mabaya zaidi tangu kichapo cha 3-0 dhidi ya Posta Rangers Januari mwaka 2022, Akonnor alitetea maguezi yake, akisema yalichochewa na uchovu wa wachezaji wake kutokana na mechi nyingi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Many people experience stress aid

AKONNOR AKUBALI KUWAJIBIKIA MATOKEO DUNI

SHEREHE YA PEP YATIWA DOA ULAYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *