#Local News

RUKU AMKOSOA OGINGA KWA KUDAI WADHIFA WA NAIBU RAIS

Baadhi ya viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya wamekosoa hatua ya kinara wa ODM Oburu Oginga kubadili msimamo na kutangaza kwamba chama hicho kinalenga wadhifa wa naibu Rais kama sehemu ya ushirikiano na chama cha UDA kwenye uchaguzi mkuu ujao, wakisema wadhifa huo utaendelea kushikiliwa na naibu Rais Kithure Kindiki.

Waziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku ambaye amezungumza mjini Embu, amekariri kuwa kamwe hawataruhusu wadhifa wa naibu rais kuponyoka eneo hilo mwaka ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RUKU AMKOSOA OGINGA KWA KUDAI WADHIFA WA NAIBU RAIS

RUTO KUELEKEA ETHIOPIA MKUTANO WA AU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *