EACC YATAKIWA KUZUIA UNYAKUAJI WA ARDHI CHEPCHOINA
Wakaazi wa ardhi ambayo imekumbwa na utata ya Chepchoina kaunti nya Trans Nzoia wameitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya maafisa wa serikali ambao wamekuwa wakinyakua mashamba yao.
Aidha wakaazi hao wamesema kuwa mgogoro huo huenda ukaleta vurugu ikiwa wizara ya Ardhi na usalama hazitaingilia kati kutatua swala hilo .
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































