BEATRICE CHEBET NJE YA UWANJA 2026
Mshindi wa nishani ya dhahabu 2 katika mbio za mita 10,000 na mita 5,000 katika mashindano ya Paris Olympics 2024 Beatrice Chebet atakuwa nje ya mashindano mwaka huu baada ya kuchukua likizo ya kujifungua.
Haya ni kulingana na tangazo la ajenti wake, likimaanisha kwamba mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 hatatetea taji lake katika mbio za World Cross Country katika jimbo la Florida nchini Marekani kutokana na likizo hiyo.
Tangazo lake la kujiondoa katika mbio hizo siku chache zilizopita liliibua uvumi, ila ajenti wake amezima uvumi huo akisema Chebet atakimbia mbio ambazo amaezitaja kuwa muhimu sana katika maisha yake, ambazo ni kuwa mama.
Hata hivyo, Chebet hatakosa mbio zozote kuu, ikizingatiwa kwamba mashindano makuu yatakuwa mwaka ujao jijini Beijing na kisha Los Angeles Olympics mwaka wa 2028.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































