#Business

KPLC YATOA SHILINGI BILIONI 3.5 KWA MAKUNDI MAALUM

Kandarasi za kibiashara zenye thamani ya shilingi bilioni 3.5 zlitolewa kwa watu walio na changamoto za kimaumbile, vijana na wanawake katika mwaka wa kifedha wa 2024-25 kutoka kwa kampuni ya kusambaza umeme KPLC

Vijana, wanawake na watu walio na changamoto hizo wanatambulika kuwa ni makundi maalum ya wanazabuni chini ya mfumo wa upatikanaji wa fursa za ununuzi serikalini (AGPO), ambao unazitaka taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti yao ya mauzo ya mwaka kwa ajili ya zabuni zinazoelekezwa kwa vikundi hivyo.

Katika taarifa, KPLC imebainisha kuwa kandarasi hizo ni nyongeza kubwa kutoka kwa shilingi milioni 614 iliyotolewa katika mwaka wa kifedha uliokamilika Juni 30, 2024. Katika mwaka wa fedha, kampuni zinazomilikiwa na vijana zilipata mgao mkubwa zaidi, ambao ni shilingi bilioni 2.2, ikifuatiwa na biashara zinazomilikiwa na Wanawake na watu wenye ulemavu wa Ksh.1.25 bilioni na Ksh.66.7 milioni mtawalia.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

KPLC YATOA SHILINGI BILIONI 3.5 KWA MAKUNDI MAALUM

PIGO LA MAJERAHA KATIKA SAFU YA ULINZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *