RUTO AMWOMBOLEZA MBUNGE WA ISIOLO SOUTH
Risala za rambi rambi zimeendelea kutolewa kuhusiana na kifo cha mbunge wa Isiolo South Tubi Bidu, aliyefariki hapo jana katika Nairobi Hospital alikokuwa akipokea matibabu.
Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii X, Rais William Ruto amemtaja Bidu kama mtumishi wa umma aliyejitolea kupigania elimu, aliyeamini katika kuimarisha jamii kupitia ujuzi na fursa.
Mbunge huyo ambaye amekuwa kwenye muhula wake wa kwanza, alikuwa mwanachama wa kamati ya mazingira, misitu na madini katika bunge la kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































