BRYNE OMONDI APONGEZA UTEUZI WA WACHEZAJI CHIPUKIZI
Kipa wa Harambee Stars, Bryne Omondi, amepongeza uteuzi wa
wachezaji chipukizi kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichoitwa na
kocha Benni McCarthy.
Omondi amesema ujio wa wachezaji wachanga ndani ya timu ya taifa
utawapa motisha vijana wengine nchini kuendelea kujituma ili
kutimiza ndoto zao za kuchezea Stars.
Miongoni mwa wachezaji wapya walioitwa ni mshambuliaji Job
Ochieng, anayesakata soka nchini Hispania na klabu ya Real Sociedad
B, ambaye alichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza katika
kampeni za kufuzu Kombe la Dunia 2026 na Aldrine Kibet anayekipiga
na klabu ya Celta Vigo
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































