#Local News

IDADI YA WALIOSAJILIWA NA IEBC KUFIKIA SASA

Ni wakenya 90,020 pekee ndio wamesajiliwa kama wapiga kura wapya katika zoezi linaloendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume hiyo, kaunti za Nairobi, Kiambu na Machakos zinaongoza kwa idadi ya waliosajiliwa kwa wapiga kura wapya 16,512, 9,917 na 4,026 mtawalia.

Kufikia Oktoba 31, jumla ya wapiga kura 15,619 walikuwa wamehamishia kura zao katika vituo vipya.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *