#Basketball #Sports

KENYA YAJIANDAA KWA 2026 GLASGOW COMMONWEALTH

Shirikisho la mpira wa vikapu kwa wachezaji wanaotumia viti vya magurudumu KWBF limeimarisha maandalizi kwa ajili ya mashindano ya kufuzu michezo ya 2026 Glasgow Commonwealth, baada ya kuandaa majaribio ya wanawake kwa wanaume katika viwango vya 3×3 na 5×5, Pamoja na kikosi cha wanawake wasiozidi umri wa miaka 25.

Majaribio hayo yaliyoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Kasarani, yaliwavutia zaidi ya wachezaji 70 kutoka zaidi ya kaunti 5, rais wa shirikisho hilo Alfred Simiyu, akitaja idadi hiyo kuwa ya kuridhisha licha ya changamoto za kiuchumi.

Vikosi vya 3×3 na 5×5 vitajiandaa kwa mashindano ya ubingwa wa Afrika chini ya shirikisho la kimataifa la IWBF jijini Luanda nchini Angola kuanzia tarehe 27 mwezi Machi hadi Aprili 4 mwaka ujao.

Ubingwa huo utabaini timu za kuwakilisha bara Afrika kwenye mashindano ya ubingwa wa Glasgow Commonwealth.

Aidha, Kenya itawasilisha timu ya wachezaji 12 wa kike katika ubingwa wa U25 jijini Kinshasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KENYA YAJIANDAA KWA 2026 GLASGOW COMMONWEALTH

IMLU YAONYESHA MADHILA DHIDI YA RAIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *