BENKI YA DUNIA YATENGA KES. 64 KUBORESHA RELI YA TRENI YA ABIRIA NAIROBI
Benki ya Dunia inatazamiwa kutumia takriban shilingi bilioni 64.5 kusaidia ukarabati wa njia ya reli ya abiria jijini Nairobi kama sehemu ya mpango mpana wa kuboresha usafiri wa mijini katika mji mkuu.
Kufuatia ripoti, mpango huo kwa sasa uko katika hatua ya kukagua dhana na ni sehemu ya mpango mkubwa unaokadiriwa kugharimu takriban shilingi bilioni 219. Kulingana na dokezo la mradi lililochapishwa kwenye tovuti ya wakopeshaji, mradi huo utajikita katika kuboresha njia ya reli kati ya CBD na Thika, kuboresha stesheni za reli, kupata mabehewa mapya ya reli na kuboresha miundomsingi mingine muhimu ili kuongeza ufanisi na uwezo.
Mkopeshaji pia atafadhili upembuzi yakinifu na kazi ya usanifu wa awali kwa mtandao wa reli ya abiria, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya uwezekano wa kusambaza umeme. Usaidizi wa ziada wa kiufundi utasaidia fursa za ufadhili wa kaboni na uanzishaji wa mifumo ya ufadhili wa uhamaji mijini, ikijumuisha uwezekano wa uwekaji dhamana wa Ushuru wa Maendeleo ya Reli.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































