FIFA YAPITISHA SHERIA MUHIMU KWA SOKA YA WANAWAKE
Timu zote zinazoshiriki mashindano ya soka ya wanawake zitahitajika kuwa na makocha au makocha wasaidizi wanawake.
Hii ni baada ya shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA, kupitisha sheria hiyo hapo jana katika mkutano wa baraza lake.
Sheria hiyo itaanza kutekelezwa katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 mwezi Septemba, na pia katika mashindano ya kombe la dunia ya wanawake mwaka ujao nchini Brazil, pamoja na makala ya 2 mashindano ya kombe la mabingwa la wanawake, awamu ya kwanza ya dimba la klabu bingwa ya wanawake ulimwenguni.
FIFA imeelezea matumaini kwamba huenda sheria ikatatua ukosefu wa makocha wanawake licha ya ukuaji wa soka ya wanawake.
Aidha, sheria hiyo itakayotumiwa katika mashindano yote ya vijana, watu wazima, timu za kitaifa na klabu, pia italazimu kuwepo na angalau wanawake wawili kwenye benchi la kiufundi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































