WAKAZI WA BWAWA LA NAIROBI WATAKIWA KUHAMA
Wakazi wanaoishi maeneo ya chini ya bwawa la Nairobi kama vile Kibra, Lang’ata, South C na Madaraka wametakiwa kuhama kufuatia kupanda kwa kiwango cha maji kwenye bwawa hilo, ambayo yanahofiwa kusababisha maafa.
Kwenye tahadhari yake, mamlaka ya raslimali za maji, WRA, imesema kiwango hicho kimefikia hali ya hatari, na kuwataka wakazi kuhamia maeneo salama mapema, huku idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini ikifikia watu 83 kufikia jana.
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, ameonya dhidi ya siasa kuingizwa kwenye tahadhari hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































