SERIKALI YATOA HAKIKISHO LA MAFUTA
Waziri wa Nishati na Petroli, Opiyo Wandayi, amewahakikishia Wakenya kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta licha ya mataifa kadhaa barani Afrika kukumbwa na uhaba.
Akizungumza kufuatia taarifa za foleni ndefu katika vituo vya mafuta katika baadhi ya nchi, Wandayi amesema Kenya haijakumbwa na upungufu wowote na inaendelea kuwa na usambazaji thabiti wa bidhaa muhimu za mafuta.
Aidha ameeleza kuwa uthabiti huo unatokana na mfumo wa usambazaji wa mafuta kati ya serikali na serikali, akibainisha kuwa kuna akiba ya kutosha ya petroli, dizeli, mafuta ya ndege, mafuta ya taa na gesi ya kupikia, huku shehena zaidi zikitarajiwa kuwasili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































