#Local News

PVK YASUTA SERIKALI KUHUSU MAFURIKO

Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya umetoa taarifa ukisoa jinsi serikali inavyoshughulikia janga la mafuriko linaloendelea, ukilitaja kuwa ni “kushindwa kwa kitaifa”.

Wakiongozwa na Mwenyekiti na Kiongozi wa Kanisa la Jesus Teaching Ministry Apostle Peter Manyuru Muungano huo umetuma rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kuonyesha mshikamano na maelfu ya waliokosa makazi kote nchini.

Viongozi hao wa kanisa wameisuta serikali kwa kile wanachokitaja kuwa ni miaka ya mipango duni, ufisadi na uzembe uliosababisha hali kuwa mbaya zaidi, wakitilia shaka uwajibikaji wa wanaosimamia rasilimali za umma

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *