TUCHEL AHOJI KIKOSI BAADA YA KIPIGO
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Thomas Tuchel, amesema sasa ana uelewa zaidi kuhusu kikosi chake licha ya kipigo cha mabao 1-0 dhidi ya Japan katika mechi ya kirafiki.
Tuchel alikuwa ameteua kikosi cha wachezaji 35 kwa mechi dhidi ya Uruguay na Japan, huku sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay ikihusisha wachezaji wa akiba ambao hawakuvutia sana.
Kocha huyo alitarajia kuwatumia wachezaji wake wa kikosi cha kwanza, lakini mipango yake ilivurugika kutokana na kuondolewa kwa baadhi ya wachezaji, hali inayozua maswali zaidi kuelekea Kombe la Dunia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































