ST. ANTONY’S YALENGA UBINGWA KISUMU
Kocha wa timu ya magongo ya St. Antony’s Kitale, Kevin Lugalia, amesema kikosi chake kitachukulia kila mechi kama fainali katika michezo ya kitaifa ya shule za upili itakayoanza Jumatatu jijini Kisumu.
Lugalia amesema timu imeimarisha maandalizi yake na inaamini ina uwezo wa kutwaa ubingwa katika mashindano hayo.
St. Antony’s imepangwa katika Kundi A pamoja na Kisumu Day, Alliance High School na Mbooni Boys, kundi ambalo kocha amesema lina ushindani mkali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































