#Local News

KAMATI YA BUNGE YAIDHINISHA FEDHA KULIPA MADENI YA NHIF

Kamati ya Bunge ya Afya imeidhinisha ombi la Wizara ya Afya la kutenga shilingi milioni 5.3 kusaidia kulipa madeni ya Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) yanayodaiwa na vituo mbalimbali vya afya.

Hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo mkubwa wa madeni unaoathiri vituo vya afya vinavyodai serikali, hali inayochangia kudorora kwa utoaji wa huduma za afya nchini.

Wabunge wamesema kuwa kulipwa kwa madeni hayo kutasaidia kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha sekta ya afya kote nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *