KIVUMBI CHATARAJIWA KATI YA GOR VS SHABANA FC
Kinyang’anyiro kikali kinatarakiwa wikendi hii katika ligi ya soka, KPL, viongozi Gor Mahia watakapovaana na Shabana FC hapo kesho ugani Nyayo.
K’Ogalo wataingia katika mtanage huo wakiwa uongozini kwa pointi 53 baada ya mechi 24, Shabana nao wakiingia uwanjani wakiwa na shinikizo baada ya kichapo mara 2 mfululizo, matokeo ambayo yamesababisha kufutwa kwa kocha wake mkuu Peter Okidi.
Kwa sasa wako katika nafasi ya 3, pointi 13 nyuma ya Gor.
Kaimu kocha wao Andrea Ongwae, anakabiliwa na kibarua cha kubadilisha matokeo ya kikosi hicho, mbali na kurejesha imani miongoni mwa wachezaji.
Kwenye mechi kati ya mwisho baina ya GOr na Shabana, timu hizo zilishindwa kuifungana mabao mwezi Januari, wakati huo timu zote zikiwa na tahadhari.
Hata hivyo, huenda mambo yakawa tofauti hapo kesho ikizingatiwa kuwa K’Ogalo wanalenga kuimarisha uongozi, huku Shabana wakilenga kujiweka sawa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































