MUSYOKA AONYA UCHAGUZI WA KIMAPINDUZI 2027
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC kulihakikishia taifa uchaguzi huru na haki mwaka ujao, akionya kuwa uchaguzi huo utakuwa wa kimapinduzi.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Musyoka amesisitiza kuwa IEBC ina fursa ya kujitenga na dhana kwamba makamishna wake ni vibaraka wa Rais William Ruto jinsi ambayo imekuwa ikidaiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Aidha, amewataka vijana kuendelea kujisajili kwa wingi kama wapiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































