#Football #Sports

KOCHA MPYA WA MOROCCO APONGEZA UAMUZI WA CAF

Kocha mpya wa taifa la Morocco, Mohamed Ouahbi, amewapongeza wachezaji wake Abaada ya uamuzi wa CAF kutoa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kutoka kwa Senegal na kuwapa Morocco.

Senegal ilishinda fainali Januari 18 mjini Rabat kwa mabao 1-0, lakini CAF iliamua kuwapokonya wachezaji wa Senegal taji baada ya wachezaji hao kuondoka uwanjani kwa ishara ya maandamano walipokuwa wakikabiliwa na penalti iliyotolewa kwa wenyeji mwishoni mwa muda wa majeruhi ya kipindi cha pili.

Baada ya wachezaji wa Senegal kurejea uwanjani Morocco walishindwa kufunga penalti, na Pape Gueye alifunga bao la ushindi katika nyongeza ya muda, akipeleka Lions of Teranga kuwa mabingwa wa taji hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *