#Football #Sports

KIVUMBI UCL: REAL MADRID vs MAN CITY, CHELSEA vs PSG

Kivumbi kinatarajiwa kushuhudiwa hii leo katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya huku timu za Chelsea na Manchester City zikitazamia kubadilisha matokeo ya mkondo wa kwanza ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali.

Saa tatu kasorobo itashuhudia Bodo Glimt wakisafiri kuelekea ureno kuchuana na Sporting Lisbon ambapo Glimt wanalenga kufuzu robo fainali haswa baada ya kushinda mkondo wa kwanza 3 – 0.

Saa tano usiku Arsenal watakaribisha Bayer Leverkusen, wakati City wakiangazia kubadili kichapo cha mkondo wa kwanza cha 3 – 0 watakapokuwa wenyeji wa Real Madrid. Chelsea nao wanatafuta mabao manne bila jibu wakati wakiwa nyumbani Stamford Bridge kukaribisha Paris St. Germain baada ya kubamizwa mabao 5-2 katika mechi yam kondo wa kwanza.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *