#Football #Sports

ITALIA WAAZIMIA KUKATA KIU CHA KOMBE LA DUNIA KWENYE MWONDOANO

Timu ya taifa ya soka ya Italia inaazimia kumaliza kijibaridi cha kukaa nje ya kombe la dunia kwa miaka 12, inapoingia katika awamu ya mwondoano ili kusaka tiketi ya kipute hicho muhimu zaidi katika ulimwengu wa soka.

Italia wataikaribisha Northern Ireland katika eneo la Bergamo, katika kinachotarajiwa kuwa semi fainali yenye ushindani wa hali ya juu, Italia ikiwa na hamu ya kuepuka kuwa nje ya dimba hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Gennaro Gatuso aliiongoza Italia kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Norway kwenye Group I, na amefanikiwa kwa kiasi kuimarisha kikosi hicho cha Azzurri kufuatia kufutwa kazi kwa Luciano Spalleti.

Hata hivyo, vichapo viwili vizito kutoka kwa Norway viliikumbusha timu hiyo jinsi imeporomoka tangu kushinda taji hilo miaka 20 iliyopita, Gatusso alipokuwa kiungo wa timu hiyo.

Tangu taji hilo la mwisho, Azzurri hawajawahi kufika awamu ya mwondoano, wakibanduliwa kwenye awamu ya makundi mwaka 2010 na 2014, kabla ya kukoseshwa fursa ya kufuzu mashindano hayo makala ya 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii, Gatusso alikiri kuwepo kwa kibarua katika kusaka tiketi ya kuingia Marekani, Mexico na Canada mwezi Juni mwaka huu.

Kikosi chake kinakabiliwa na majeraha kwa wachezaji muhimu, akiwemo Sandro Tonali wa Newcastle, na Federico Chiesa wa Liverpool, huku mshambulizi wa Atalanta Gianluca Scammacca, na mabeki wa kati Alessandro Bastoni na Gianluca Mancini wakijaribu kupona.

Gattuso pia aliweka wazi kwamba beki wa Arsenal Riccardo Calafiori hakuwa akihisi vizuri alipowasili katika kambi ya mazoezi.

Ushindi wao hii leo utawakutanisha na mshindi kati ya Wales na Bosnia-Herzegovina katka kizuizi cha mwisho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *