WAFANYAKAZI WA VIWANJA VYA NDEGE KUGOMA TENA
Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ina muda wa siku 6 kushughulikia malalamishi ya wafanyakazi wa viwanja hivyo ambao wameonya kuwa watagoma na kutatiza shughuli katika viwanja hivyo iwapo ilani yao itapuuzwa.
Kwenye makataa ya siku 7 yaliyotolewa hapo jana, muungano wa wafanyakazi hao, KAWU, unataka mamlaka hiyo itekeleze makubaliano yaliyotiwa saini mwezi jana, mbali na kumrejesha kazini mfanyakazi aliyefutwa kazi Desemba mwaka jana jinsi mahakama ilivyoagiza.
Katibu mkuu wa KAWU Moss Ndiema, amelalamikia kufutwa kazi kwa mfanyakazi mwingine wiki jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































