UTOAJI WA VITAMBULISHO WAONGEZEKA NCHINI
Serikali imeripoti ongezeko la utoaji wa vitambulisho vya kitaifa, ikisisitiza umuhimu wake katika utambuzi wa raia na upatikanaji wa huduma muhimu.
Zaidi ya vitambulisho milioni 4.1 vimetolewa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, huku milioni 1.6 vikitolewa katika miezi sita iliyopita, sambamba na kuanzishwa kwa mfumo mpya ulio salama na wenye uwajibikaji zaidi.
Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Uhamiaji, Belio Kipsang, serikali imeondoa mfumo wa kamati uliokuwa ukilalamikiwa kwa ubaguzi na kuwapa machifu jukumu la uthibitishaji, huku vyombo vya usalama vikiendelea na uhakiki wa ziada.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































