MUDAVADI ATETEA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA KAUNTI YA NAIROBI.
Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi, ametetea na kueleza athari pana za makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na Kaunti ya Nairobi.
Mudavadi amesema mfumo huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa miundombinu ya jiji, utoaji wa huduma na ushindani wake kimataifa.
Akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali, Mudavadi alisema makubaliano kati ya utawala wa William Ruto na Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja, ni ushirikiano wa kimkakati unaolenga kutatua changamoto za muda mrefu za mijini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































