#Local News

RUTO AAHIDI KUILINDA HOSPITALI YA NAIROBI DHIDI YA WAHUJUMU

Rais William Ruto amevunja ukimya wake kuhusu mzozo unaoikumba The Nairobi Hospital, akiahidi kuilinda dhidi ya watu aliowataja kuwa matapeli wanaotaka kuihujumu.

Kwa mujibu wa Rais, baadhi ya maafisa wa hospitali hiyo walimfikia wakitaka aingilie kati kuhusu madai ya jaribio la kuiteka, ombi ambalo amesema atalishughulikia kwa dhati.

Wakati huo huo, Ruto amesema ameagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wanaohusishwa na vurugu hizo, akisisitiza kuwa hospitali hiyo lazima ilindwe ili iendelee kuwahudumia Wakenya ipasavyo huku akisuta upinzani kwa kile alichokitaja kuwa kukosa ufahamu dhidi ya kinachoendelea katika hospitali ya Nairobi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *