RUTO AANZA ZIARA MAGHARIBI
Wakazi wa eneo la Magharibi mwa nchi wanatarajia kunufaika na uzinduzi wa miradi ya maendeleo utakaoongozwa na Rais William Ruto, ambaye ameanza ziara yake ya siku 4 katika kaunti zote 4 za eneo hilo.
Katika kaunti ya Busia anakoanzia ziara hiyo, Rais atazindua ujenzi wa barabara za Mundere Okando-Sio Port-Nangina- Matayos-Namusira-Nasewa, na Matayos-Nangina-Sio-Port-Mubaka, na masoko pamoja na mradi wa nyumba za bei nafuu.
Kulingana na ratiba ya zaiara hiyo, Rais atazindua mradi wa umeme katika kaunti ya Kakamega, na kuweka msingi wa ujenzi wa soko la kisasa la Malaha miongoni mwa miradi mingine kabla ya kuzuru Bungoma na Vihiga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































