#Football #Sports

MABADILIKO YA DAKIKA ZA MWISHI KIKOSINI HARAMBEE STARS

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanaume Harambee Stars, Benni McCarthy, amelazimika kukifanyia mageuzi kikosi chake dakika za mwisho kutokana na majeraha kwa takribani wachezaji 10 akiwemo nahodha Michael Olunga.

Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda lango Brian Omondi, mabeki Eric Ouma, Joseph Okumu, Sylvester Owino na Collins Sichenje.

Aidha, Tylor Onyango, Andry Gitau, Adam Wilson, na John Oyunga pia wameachwa nje kutokana na majeraha.

Waliojumuishwa kikosini dakika za mwisho ni pamoja na kipa Farouk Shikalo, beki Mike Kibwage na mshambulizi Ben Stanley.

Stars wako nchini Rwanda ambako wanajiandaa kwa mashindano ya FIFA Series, yatakayowapa fursa ya kujiandaa kwa mashindano ya taifa bingwa barani Afrika, AFCON 2027.

Mechi yao ya ufunguzi itakuwa dhidi ya Estonia Ijumaa wiki hii.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *