#Football #Sports

CARRICK AMTAKA TUCHEL KUWAPA NAFASI WACHEZAJI WA MAN UNITED

Kocha wa muda Manchester United Michael Carrick amemtaka kocha wa timu ya taifa ya England Thomas Tuchel kuwapa nafasi wachezaji wa klabu hiyo kuthibitisha uwezo wao kuelekea Kombe la Dunia.

Carrick amewataja Harry Maguire, Luke Shaw na Kobbie Mainoo kama wachezaji wanaostahili kupewa nafasi, akibainisha kuwa hawajateuliwa tangu Tuchel achukue usukani wa timu hiyo Januari 2025.

Ameongeza kuwa hali hiyo inaonyesha kushuka kwa kiwango cha Manchester United katika miaka ya hivi karibuni, huku akimhimiza Tuchel kuwatumia wachezaji hao katika mechi za kirafiki dhidi ya Japan na Uruguay baadaye mwezi huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

CARRICK AMTAKA TUCHEL KUWAPA NAFASI WACHEZAJI WA MAN UNITED

VIJANA WATARAJIA AJIRA ZA SGR

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *