GACHAGUA AMWEKA DUALE MBIO KUHUSU SHA
Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ameendeleza madai yake kuhusu ufisadi katika bima ya afya ya jamii SHA, akisema waziri wa afya Aden Duale ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni moja inayoshukiwa kutumika kwenye ufujaji wa shilingi bilioni 104 kwenye bima hiyo.
Akizungumza kwenye ziara ya muungano wa upinzani eneo la Ukambani, Gachagua amesema kuwa kampuni hiyo ni mojawapo ya kampuni zilizopewa zabuni ya kusimamia mfumo wa SHA.
Hata hivyo, Duale amepuzilia mbali madai hayo, akimtuhumu Gachagua kwa madai ya kuitisha hongo kutoka kwa kampuni hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































